Ujumbe
wa malaika wa kwanza ni wito wa kumwabudu Mungu Muumbaji. Kwa kweli,
lugha yenyewe inatukumbusha sisi juu ya maneno yale yaliyotumika katika
amri ya nne. Malaika wa kwanza asema hivi: “Mcheni Mungu, na kumtukuza,
kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya
mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji” (Ufunuo 14:7). Vilevile,
amri ya nne yatuambia sisi kumwabudu Mungu kwa sababu yeye ni Muumbaji
wa vitu vyote mbinguni, duniani, na baharini. Yatuambia kwamba siku ya
pekee ambayo Mungu ameitenga kwa ajili ya ibada ni siku ya saba ya juma
- siku ya Sabato yake takatifu (angalia Kutoka 20:8-11).
Sunday, September 7, 2014
UJUMBE WA MALAIKA WA PILI
Ujumbe wa malaika wa pili ni huu: “Umeanguka, umeanguka Babeli, mji ule
ulio mkubwa, maana ndio uliowanywesha mataifa yote mvinyo ya ghadhabu ya
uasherati wake” (Ufunuo 14:8). Babeli lilikuwa ni taifa katika Agano la
Kale ambalo liliishambulia Israeli, yaani, watu wa Mungu, na kuwachukua
mateka. Babeli lilikuwa ni taifa lililojaribu kuifutilia mbali ibada
ya Mungu wa kweli wa mbinguni na mahali pake kuweka miungu ya kipagani.
Na hivyo Babeli ikawa ishara iliyowakilisha majeshi
yote yatakayowapinga watu wa Mungu katika siku za mwisho. Kwa hiyo
malaika huyu wa pili anasema kwamba Babeli umeanguka kwa sababu
umeyafanya mataifa yote ya dunia kunywa mvinyo ya uasherati wake, yaani,
hiyo ni njia ya kusema kwamba majeshi yanayopigana na Mungu katika siku
hizi za mwisho yatajaribu kumlazimisha kila mmoja kutoa utii wake kwa
majeshi hayo kuliko kwa Mungu. Imewakilishwa kama “uasherati,” au
uzinzi. Kutokumtii Mungu kunaonyeshwa katika Biblia kama uzinzi wa
kiroho, jambo hili lote linatufikisha kwenye hoja ya utii.
UJUMBE WA MALAIKA WA TATU
Malaika
wa tatu anatangaza hivi: “Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na
sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika
mkono wake, yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu
iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira
yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu,
na mbele za Mwana-Kondoo” (Ufunuo 14:9,10). Maneno haya machache ni onyo
muhimu kabisa ambalo Mungu amepata kulitoa katika Biblia. Anatuonya
sisi dhidi ya kuisujudu mamlaka hii ambayo inapingana naye, naye
anatuonya sisi tusipokee chapa yake. Mamlaka hii ni nani au ni kitu
gani na alama yake ni alama gani?
Je umewahi kumuomba MUNGU akufunulie ili uweze kuepukana na mapigo 7?
Tafakari.
Je umewahi kumuomba MUNGU akufunulie ili uweze kuepukana na mapigo 7?
Tafakari.
Subscribe to:
Posts (Atom)