Sunday, March 19, 2017

CHUO KIKUU CHA MUNGU


FUNGU LA MAANDIKO:
Maana hekima ya dunia hii ni upuzi mbele za Mungu. Kwa maana imeandikwa, Yeye ndiye awanasaye wenye hekima katika hila yao
1 Wakorintho 3:19

----------------
Wanapojitahidi kujiweka wenyewe katika hali ya kustahili kuwa watendakazi pamoja na Mungu, mara kwa mara watu hujiweka katika nafasi ambazo hatimaye huwafanya wasistahili kabisa kuumbwa na kutengenezwa kwa namna ambayo Bwana angependa wawe.
Kwa namna hiyo, hawaonekani kama Musa kuchukua mwonekano wa Mungu.
Kwa kujikabidhi wenyewe kwa nidhamu ya Mungu, Musa alikuwa mfereji uliotakaswa ambao kwa kupitia kwa huo, Bwana aliweza kufanya kazi. Hakusita kubadilisha njia yake kwa kuchukua ile ya Bwana, hata ingawa iliongoza katika mapito mageni, kwenye njia ambazo zilikuwa hazijajaribiwa kabla….
Kilichomwezesha Musa kushinda dhidi ya maadui zake haikuwa mafundisho ya shule za Misri, bali imani ya kudumu, imani isiyolegea, imani ambayo haikushindwa nyakati za majaribu makali zaidi…. Musa alitenda kama aonaye yasiyoonekana.
Mungu hatafuti watu wenye elimu kamilifu… Bwana anataka watu wathamini fursa ya kuwa watendakazi pamoja na Mungu – watu watakaomheshimu kwa kuwa na utii dhahiri kwa masharti yake bila kujali dhana zilizoingizwa akilini mwao kabla…
Wengi wanaotafuta ubora kwa ajili ya kazi hii ya Mungu iliyotukuka kwa kukamilisha elimu yao kwenye shule za wanadamu, wataona kwamba wameshindwa kupata masomo ya muhimu zaidi ambayo Bwana angewafundisha. Kwa kupuuzia kujisalimisha wenyewe kwa fikra za Roho Mtakatifu, kwa kutoishi katika kutii masharti yote ya Mungu, ubora wao wa kiroho unadhoofika…
Kwa kutojihudhurisha wao wenyewe kwenye shule ya Kristo, wanakuwa wamesahau sauti ya Mwalimu na hawezi kuongoza mpango wao.
Watu wanaweza kupata ujuzi na ufahamu wote unaohitajika kuwekwa ndani ya mwalimu aliye mwanadamu; lakini bado ipo hekima kubwa zaidi ambayo Mungu anahitaji wawe nayo. Kama ilivyokuwa kwa Musa, ni lazima wajifunze upole, unyenyekevu wa moyo na waache kutumainia nafsi.
Mwokozi wetu yeye mwenyewe, akiwa amechukua jaribu la ubinadamu, alikiri kwamba kwa namna alivyokuwa yeye mwenyewe hangeweza kufanya neno lolote.
Ni lazima sisi pia tujifunze kwamba hakuna nguvu katika ubinadamu peke yake.
Mtu anaweza kuwa na ufanisi pale tu anapokuwa mshirika wa tabia ya Mungu.
Rehema za Bwana ni MPYA KILA SIKU ASUBUHI
MAOMBOLEZO 3: 22-23