Manabii
wa uongo wanaendelea kuwadanganya watu eti watakatifu au wateule au
waliompokea Yesu hawatapitia katika dhiki isipokuwa watanyakuliwa ndipo
dhiki kuu ifate kwa wadhambi....
Yani wanasema Ufufuo utaanza alafu dhiki kuu ndo inafata...
Huu ni uongo mkubwa.
Yani wanasema Ufufuo utaanza alafu dhiki kuu ndo inafata...
Huu ni uongo mkubwa.
JE YESU ANASEMAJE?
JE BIBLIA INASEMAJE?
Mathayo 24:
9 Wakati huo watawasaliti ninyi mpate dhiki, nao watawaua; nanyi mtakuwa watu wa kuchukiwa na mataifa yote kwa ajili ya jina langu.
9 Wakati huo watawasaliti ninyi mpate dhiki, nao watawaua; nanyi mtakuwa watu wa kuchukiwa na mataifa yote kwa ajili ya jina langu.
10 Ndipo wengi watakapojikwaa, nao watasalitiana, na kuchukiana.
13 Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka.
BIBLIA INASEMA
Watakatifu watachukiwa kwa ajili ya jina la Yesu
Watakatifu watachukiwa kwa ajili ya jina la Yesu
Swali ni watu gani wanaochukiwa kwa ajili ya jina la Yesu kama sio wale wanaoyafata mapenzi ya Mungu?
HII inaonesha kuwa watakatifu watakuwa katika dhiki kuu
Katika dhiki hiyo mwenye kuvumilia ndiye atakayeokoka.. Bila shaka
wenye kuvumilia ni wale walio na Yesu maana wataipitia dhiki kuu.
TENA BIBLIA INASEMA KATIKA DHIKI HIYO SIKU ZISINGELIFUPIZWA ASINGEOKOKA
MTU YEYOTE MAANA WATAKATIFU WATATESWA KATIKA DHIKI HIYO.
Mathayo 24: 21 Kwa kuwa wakati huo kutakuwapo dhiki kubwa, ambayo
haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala
haitakuwapo kamwe.
22 Na kama siku hizo zisingalifupizwa, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule zitafupizwa siku hizo.
JE BAADA YA DHIKI KUU NI NINI KITAFATA?
Mathayo 24: 29 Lakini mara, baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa
giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka mbinguni, na
nguvu za mbinguni zitatikisika;
30 ndipo itakapoonekana ishara
yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu
watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya
mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi.
Biblia inasema itaanza dhiki na wale watakao vumilia hadi mwisho katika
dhiki kuu ile pasipo kumkana Yesu wataokoka Yesu akija kuwachukua.
JE WATAOSHINDA KATIKA DHIKI KUU NA KWENDA MBINGUNI, JE HUKO MBINGUNI WATASEMAJE JUU YAO?
Ufunuo 7:
13 Akajibu mmoja wa wale wazee akiniambia, Je! Watu hawa waliovikwa mavazi meupe ni akina nani? Na wametoka wapi?
13 Akajibu mmoja wa wale wazee akiniambia, Je! Watu hawa waliovikwa mavazi meupe ni akina nani? Na wametoka wapi?
14 Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, Hao ndio wanatoka
katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe
katika damu ya Mwana-Kondoo.
Shetani atatafta kila njia ya kutaka watu wapigwe chapa ya mnyama
Lakini habari njema ni kwamba wale watakao kuwa wamempokea Yesu wa kweli watashinda.
Lakini habari njema ni kwamba wale watakao kuwa wamempokea Yesu wa kweli watashinda.
MUNGU AKUBARIKI UNAPOUKIMBIA UONGO.