Friday, July 17, 2015

TUMEFIKA MWISHO WA ULIMWENGU

HABARI ILIYOTIKISA  ULIMWENGU.
Sasa Ushoga(Ndoa ya jinsia moja)ni halali kisheria nchini Marekani. Maelfu ya waandamanaji wamshangilia Obama kwa kuwapa walichokuwa wakikisubiri kwa hamu.
Wapenzi wa Blog hii "TUYACHUNGUZE MAANDIKO" ndani ya wiki iliyopita ulimwengu ulitikiswa kwa habari kutanda vyombo vya Habari kuhusu uhalarishwaji wa ndoa ya jinsia nchini Marekani.
Wapenzi, kama ilivyokuwa kipindi cha Sodoma na Gomora, ndiko dunia ilikufikia. Alama za nyakati zinazidi kusonga; unabii wazidi kutimia taratibu lakini kwa uhakika.
Hili ambalo limetendeka Marekani linaakisi unabii unaopatikana katika Biblia (Warumi 1:24,26,27): "Kwa ajili ya hayo MUNGU Aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, hata waufuate uchafu, hata kuvunjiana heshima miili yao...hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili; wanaume nao vivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa..." Wapenzi, YESU Alituambia "...myaonapo hayo yote, tambueni Yu karibu milangoni" Mat 24:33 Mpenzi msomaji, inua macho yako juu, rekebisha mahali ulipoanguka kiroho na umrejee Mwokozi kabula haijaja ile siku ya ghadhabu kuu ya kuungamiza ulimwengu huu.
Sikia YESU Anavyokuambia; "Naja upesi. Shika sana ulichonacho, asije mtu Akaitwaa taji yako" Uf 3:11