Saturday, December 28, 2013

UJASILI NA MALI (UJASILIAMALI)

Hofu ni tatizo kubwa maishani mwetu, maneno yafuatayo yakujaze nguvu na kukupa mwongozo mpya kwenye Ujasiliamali.
(Nachagua kutokuwa mwananchi wa kawaida. Ni haki yangu kuamua kutokuwa mtu wa kawaida nikiweza. Nitatafuta fursa na siyo usalama, sitamani kuwa mtu wa kufugwa, ambaye nimeshushwa mpaka kufikia kiwango cha kusaidiwa na serikali. Nataka kuhatarisha na kujaribu makuu japo kwa mahesabu na tahadhari, niote ndoto na kufanya mambo, nishindwe au nifanikiwe. Nina pendelea zaidi changamoto za maisha kuliko kuhakikishiwa kuishi kwa kawaida. Ninapendelea furaha kuu ya kuridhika kwa kufanikisha kitu kuliko hali ya kupenda kila kitu kiwe shwari tu katika hali ya ukamilifu. Sitamwogopa bwana yeyote wala sitampigia goti rafiki yeyote. Ni urithi wangu kusimama imara, kwa fahari, bila woga wowote, huku nikiwaza kutenda sawasawa na nipendavyo mwenyewe na mwisho wa siku niseme, hiki kitu nimefanya mwenyewe)

Bwana akubariki, nikutakie maisha mema.