Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa kwa jinsi ya ajabu na ya kutisha. Matendo yako ni ya ajabu, Na nafsi yangu yajua sana. Zaburi 139:14
Mtunga zaburi alisema, "nimeumbwa kwa jinsi ya ajabu na ya kutisha" Mungu ametupatia welekevu na uwezo wa akili na mwili, ambao ni wajibu wetu sote kuutunza katika hali iliyo bora sana.
Inatupasa tutumie kwa hali ya juu uwezo na talanta tulizopewa na Mungu. Wote wanaodhofisha uwezo wao kimwili, kiakili na kimaadili kwa ulafi, ulevi, Uzinzi, uvutaji sigara na kahawa, uvaaji usiofaa na uvunjaji wa sheria za afya kwa namna yo yote ile itawabidi watoe hesabu zao kwa Mungu kwamazuri yote ambayo wangetenda endapo wangekuwa wamezishika sheria.
Mungu anasema "ninyi si mali yenu wenyewe" Ninyi ni mali ya Mungu. Fidia yenu ilimgarimu uhai Mwana wa Mungu... Ni lazima wote wafikilie ukuu wa dhabihu iliyotolewa.
Katika maneno ya mtume Paulo mna maana ya kina: "Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, na ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana. Wala msifuatishe namna ya dunia hii: bali ,mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema ya kumpendeza, na ukamilifu"Rum. 12:1,2. Hakuna anayeweza kuleta heshima kwa Mungu akiendeleza mtindo wa maisha utakaoleta uharibifu kwa mwili na roho. Dhabihu yetu inapasa iwe takatifu isiyo na mawaa. Hii ndiyo huduma yenye maana kwa kila mmoja. Sisi tu kazi ya Mungu, jengo la Mungu.....
Mungu anatutaka tumheshimu yeye vyote tulivyo navyo.
MUNGU AKUBARIKI SANA!