Friday, January 8, 2016

JE...... NI KIPI KITAKACHOANZA KATI YA DHIKI KUU NA UFUFUO?

Manabii wa uongo wanaendelea kuwadanganya watu eti watakatifu au wateule au waliompokea Yesu hawatapitia katika dhiki isipokuwa watanyakuliwa ndipo dhiki kuu ifate kwa wadhambi....
Yani wanasema Ufufuo utaanza alafu dhiki kuu ndo inafata...
Huu ni uongo mkubwa.
JE YESU ANASEMAJE?
JE BIBLIA INASEMAJE?
Mathayo 24:
9 Wakati huo watawasaliti ninyi mpate dhiki, nao watawaua; nanyi mtakuwa watu wa kuchukiwa na mataifa yote kwa ajili ya jina langu.
10 Ndipo wengi watakapojikwaa, nao watasalitiana, na kuchukiana.
13 Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka.
BIBLIA INASEMA
Watakatifu watachukiwa kwa ajili ya jina la Yesu
Swali ni watu gani wanaochukiwa kwa ajili ya jina la Yesu kama sio wale wanaoyafata mapenzi ya Mungu?
HII inaonesha kuwa watakatifu watakuwa katika dhiki kuu
  Katika dhiki hiyo mwenye kuvumilia ndiye atakayeokoka.. Bila shaka wenye kuvumilia ni wale walio na Yesu maana wataipitia dhiki kuu.
TENA BIBLIA INASEMA KATIKA DHIKI HIYO SIKU ZISINGELIFUPIZWA ASINGEOKOKA MTU YEYOTE MAANA WATAKATIFU WATATESWA KATIKA DHIKI HIYO.
Mathayo 24: 21 Kwa kuwa wakati huo kutakuwapo dhiki kubwa, ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe.
22 Na kama siku hizo zisingalifupizwa, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule zitafupizwa siku hizo.
JE BAADA YA DHIKI KUU NI NINI KITAFATA?
Mathayo 24: 29 Lakini mara, baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka mbinguni, na nguvu za mbinguni zitatikisika;
30 ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi.
  Biblia inasema itaanza dhiki na wale watakao vumilia hadi mwisho katika dhiki kuu ile pasipo kumkana Yesu wataokoka Yesu akija kuwachukua.
JE WATAOSHINDA KATIKA DHIKI KUU NA KWENDA MBINGUNI, JE HUKO MBINGUNI WATASEMAJE JUU YAO?
Ufunuo 7:
13 Akajibu mmoja wa wale wazee akiniambia, Je! Watu hawa waliovikwa mavazi meupe ni akina nani? Na wametoka wapi?
14 Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, Hao ndio wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-Kondoo.
  Shetani atatafta kila njia ya kutaka watu wapigwe chapa ya mnyama
Lakini habari njema ni kwamba wale watakao kuwa wamempokea Yesu wa kweli watashinda.
MUNGU AKUBARIKI UNAPOUKIMBIA UONGO.