Tuesday, November 19, 2013

UPENDO USIOPIMIKA

Nivigumu sana kuamini habari hii, mtu kufa kwaajili ya mwingine, nawakati furani inakuwa vigumu kuelewa.
Unajua tulipoanguka dhambini tu, neno linasema ilipaswa tufe mara! Mwanzo 2:17 'mtakufa hakika'

Utajiuliza kwanini basi wale wazazi wetu hawakufa siku ileile? hili ndo swali la wengi, Mwanzo 3:15 Adam akaahidiwa ukombozi, kwakuwa uzao wa mwanamke unaotajwa hapo ni Yesu Mwokozi wetu.

             KILIFANYIKA NINI HASA?
Badala ya kufa mwanadamu kifo cha milele, Yesu akafa kwaajili yetu, nijambo la kumshukuru sana Bwana na Mwokozi wetu Yesu kristo. je ni nani anaye weza kufanya kama Yesu? Alichukua udhaifu wetu, na hakulizika kwamba mwanadamu apotee milele.
Isaya 53:3-9 'Kwakupigwa kwake sisi tumepona'
Yesu anasihi leo tumpe maisha yetu, anaweza kutuokoa na dhambi zetu. haijarishi tuna dhambi kiasi gani yeye yuko kwaajili ya kuokoa.

Ninatamani siku moja kuishi na Mwokozi wetu katika makao ya milele, hebu liwe wazo lako nawe mpenzi msomaji wa blog hii.
          BWANA AKUBARIKI SANA